Mahakama moja Beijing mwaka 2022 “ilimhukumu mshtakiwa wa Uingereza alipofikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza … kutumikia kifungo cha miaka mitano kwa kosa la kupata taarifa za kijasusi kinyume cha sheria kwa ajili ya wahusika walioko nje ya nchi,” msemaji wa wizara ya mambo ya nje Wang Wenbin alisema.
Baada ya kukata rufaa, aliongeza, hukumu yake ilibakia kama ilivyo mwezi Septemba.
Jarida la The Wall Street lilitangaza habari hizo mara ya kwanza kuhusu kesi ya Ian Stones siku ya Alhamisi. Lilisema familia yake na vyanzo vingine, vilisema kuwa mfanyabiashara huyo wa Uingereza alitoweka mwaka 2018 baada ya miongo kadhaa ya kufanya kazi nchini China.
Akiulizwa kuhusu ripoti hiyo Ijumaa, Wang, akimuelezea Stones kwa jina lake la Kichina, alisema kuwa “mahakama ilisikiliza keshi hiyo kwa mujibu wa sheria.
Beijing, alisema, “ilihakikisha inampa haki mbalimbali za kisheria zinazostahili” kwa mfungwa na ilipanga maafisa wa Uingereza kumtembelea na kuhudhuria kesi yake.
“China ni nchi inayoongozwa kwa mujibu wa sheria,” Wang alisema.
“Vyombo vya mahakama vinahimiza kesi kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria, kulinda haki na maslahi ya kisheria ya raia wa China na wageni,” aliongeza.
Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP.