Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 00:46

China na Uswizi walenga kuimarisha ushirikiano wa kibiashara.


Waziri Mkuu wa China Li Qiang na Rais wa Uswizi Viola Amherd wakia mjini Bern, Uswizi, Jumatatu Januari 15, 2024.
Waziri Mkuu wa China Li Qiang na Rais wa Uswizi Viola Amherd wakia mjini Bern, Uswizi, Jumatatu Januari 15, 2024.

 China na Uswizi Jumatatu wamekubaliana kuharakisha mazungumzo yanayolenga kuimarisha ushirikiano wa kibiashara, pamoja na kurahisisha usafiri wa watu kati ya mataifa yote mawili, chombo cha habari cha China kimeripoti.

Bern na Beijing wamekubaliana kuanzishwa haraka kwa mazungmzo rasmi yanayolenga kuimarisha biashara huru iliyoanza 2013, shirika hilo la habari la Xinhua limeongeza.

China pia imekubali raia wa Uswizi kuingia bila kuhitaji visa za kusafiria. Makubaliano hayo yamefanyika yakiwa ya kwanza ya ngazi ya juu, tangu kumalizika kwa janga la COVID-19.

Ujumbe wa China uliongozwa na Waziri Mkuu Li Quiang, wakati akikaribishwa na Rais wa Uswizi ambaye pia ni waziri wa Ulinzi Viola Amherd, mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Zurich, Jumapili.

Wengine walioshiriki kwenye kikao cha Jumatatu ni pamoja na waziri wa Fedha wa Uswizi Guy Parmelin, na, mwenzake wa China Wang Wentao, Gavana wa Benki Kuu ya China, pamoja na maafisa wengine wa ngazi za juu kutoka serikali zote mbili.

Forum

XS
SM
MD
LG