Matukio hayo yamehusisha mapigano ya kijeshi, wakati New Delhi, na Beijing, zikifanya mfululizo wa mazungumzo ya kidiplomasia na kijeshi kutatua mzozo wao mbaya zaidi wa kijeshi katika miongo kadhaa.
Hakuna vifo vilivyoripotiwa katika matukio hayo. Takriban wanajeshi 20 wa India na wanajeshi wanne wa China waliuwawa katika mapigano ya eneo hilo miaka miwili iliyopita, katikati ya 2020.
Mapigano katika eneo la Ladakh, India, ambayo sasa yanajulikana yalitokea Novemba, 2022, yanaonyesha kuwa mivutano kwenye mpaka huo usio na mstari rasmi wa mpaka imeendelea kwa muda mrefu zaidi kuliko ilivyoripotiwa hapo awali.
Forum