China yaomboleza kifo cha Waziri Mkuu wa zamani Li Keqiang

Mwili wa Waziri Mkuu wa zamani wa China Li Keqiang ukiagwa na Rais wa China Xi Jinping.

China inaomboleza kifo cha Waziri Mkuu wa zamani  Li Keqiang, ambaye wakati mmoja alidhaniwa kwamba angekuwa rais wa nchi hiyo kabla ya Xi Jingping kuchukua hatamu za uongozi.

Bendera zimepepea nusu mlingoti mjini Beijing leo alhamisi.

Li, aliyebobea katika maswala ya uchumi na mzungumzaji mzuri wa kiingereza, alifariki dunia wiki iliyopita mjini Shanghai, akiwa na umri wa miaka 68.

Kifo chake kimetokea miezi michache baada ya kujiuzulu kutoka nafasi ya pili ya uongozi wa China.

Li amekuwa mtetezi wa ukombozi wa kisiasa na mabadiliko ya kiuchumi lakini alikuwa ametengwa katika mfumo wa utawala wa Rais wa China Xi Jinping aliyekuwa na madaraka ya kusimamia karibu kila kitu.

Rais wa China Xi Jinping

Chama cha kikomunisti kinachotawala nchini China, kimesema katika taarifa rasmi ya kuomboleza kwamba Li alikuwa kiongozi aliyebobea na mwaminifu kwa chama.