Hali hiyo ilijitokeza baada ya waziri wa mambo ya kigeni wa China Wang Yi kufanya vikao na maafisa wa ngazi ya juu wa Marekani mjini Washington, kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya mataifa yote mawili. Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken alifanya mazungumzo na mwenzake wa China Wang Yi, yakiwa ya kwanza ya moja kwa moja ndani ya Marekani katika miaka ya karibuni.
Ijumaa Rais Joe Biden alikutana na Wang ili kuhimiza umuhimu wa uwajibikaji kwenye ushindani kati ya Marekani na China. Maafisa kutoka mataifa yote mawili walizungumzia masuala tofauti yakiwemo vita vya Israel na Hamas, vita vya Russia na Ukraine, tatizo la dawa za kulevya aina ya fentanyl, pamoja na mzozo wa bahari ya South China Sea.
Washington imeomba China itumie ushawishi wake kwa Iran, ili kuzuia kuendelea kwa ghasia Mashariki ya Kati.
Forum