Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 02:57

Waziri Mkuu wa Australia kuzuru China mwishoni mwa wiki


Waziri mkuu wa Australia Anthony alipokuwa ametembea Marekani Oct. 25, 2023, mjini Washington.
Waziri mkuu wa Australia Anthony alipokuwa ametembea Marekani Oct. 25, 2023, mjini Washington.

Waziri mkuu wa Australia Anthony Albanese Jumamosi anaanza ziara ya siku 4 nchini China, ikiwa ya kwanza ya kiongozi wa taifa hilo tangu 2016.

Ingawa suala la kuimarisha mahusiano kati ya mataifa hayo mawili huenda likawa juu kwenye ajenda, wachambuzi wanasema kwamba Albanese pia anatarajiwa kuzungumzia kuhusu tofauti zilizopo kati ya Beijing na Canberra.

“Bado kuna katazo la Kamba (lobster) na nyama kutoka Australia, kuna suala la ushuru wa mvinyo kutoka Australia pia,” amesema Benjamin Herscovitch ambaye ni mhadhiri wa chuo kikuu cha kitaifa cha Australia.

Ziara ya Albanese inafanyika muda mfupi baada ya China kuondoa vikwazo kwenye bidhaa kadhaa za Australia, kama vile makaa, mbao na betri katika miezi ya karibuni.

Pia inafuatia taarifa kwamba China na Australia wamekubaliana kusitisha mzozo wa upelekaji mvinyo uliokuwa mbele ya shirika la kimataifa la biashara WTO, wakati Beijing ikitathmini ushuru mpya, utakaodumu kwa takrian miezi tano.

Forum

XS
SM
MD
LG