China ina wasiwasi Marekani kujiondoa katika makubaliano ya Paris

Guo Jiakun

Serikali China inasema ina wasiwasi kuhusu tangazo kwamba Marekani inajiondoa katika mkataba wa hali ya hewa wa Paris.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Guo Jiakun amesema China inajibu kikamilifu mabadiliko ya hali ya hewa na itahimiza kwa pamoja mabadiliko ya kimataifa ya kijani kibichi na kaboni.
Rais Donald Trump kwa mara nyingine tena aliiondoa Marekani katika mkataba wa hali ya hewa wa Paris mnamo Jumatatu akiondoa mtoaji mkubwa wa kaboni duniani kutokana kwa juhudi za kimataifa za kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa kwa mara ya pili katika muongo mmoja.

Rais Donald Trump akisaini amri za kiutendaji katika ofisi ya Oval ya White House, Jumatatu Jan 20, 2025, Washington, DC. AP Photo/Evan Vucci)

Dunia sasa iko kwenye kasi ya ongezeko la joto duniani la zaidi ya nyuzi joto 3 kufikia mwisho wa karne hii, kulingana na ripoti ya hivi majuzi ya Umoja wa Mataifa, kiwango ambacho wanasayansi wanaonya kwamba kingeweza kusababisha athari mbaya kama vile kupanda kwa kina cha bahari, mawimbi ya joto, na dhoruba kali.