Baada ya mjadala mkali katika baraza la chini la bunge, wabunge 330 walipiga kura kuunga mkono mswada wa “wagonjwa mahututi watu wazima (wanaokaribia kufa) na wabunge 275 wakipinga.
Chini ya mswada huo watu wenye matatizo ya akili, wagonjwa watu wazima wanaokaribia kifo nchini Uingereza na Wales ambao wametathiminiwa na madaktari kuwa na hadi miezi sita ya kuishi waweze kupewa haki ya kuchagua kumaliza maisha yao kwa msaada ya kitabibu.
Wale wanaounga mkono mswada huo wamesema inahusiana na ufupishaji kifo kwa wale ambao ni wagonjwa mahututi na kuwapa udhibiti zaidi.
Lakini wapinzani wamesema wagonjwa wenye hali tete wanaweza kuhisi haja ya kumaliza maisha yao kwa hofu ya kuwa mzigo kwa familia zao na jamii, badala ya uzima wao.
Wengine wameelezea wasiwasi kwama hakukuwa na muda wa kutosha wa kutathimini mswaada huo kabla ya kupiga kura.