Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 17:56

Uingereza kutadhmini upya ushirikiano wake wa kiuchumi na China


Waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza , David Lindon Lammy.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza , David Lindon Lammy.

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza David Lammy, hivi karibuni anatarajiwa kutembelea Beijing na Shanghai, ikiwa ziara ya ngazi ya juu zaidi nchini China tangu chama cha Labour kilipoingia madarakani.

Wachambuzi wanasema wakati wa ziara hiyo, watakuwa wakiangalia dalili za kufufuliwa kwa ushirikiano kati ya Uingereza na China, ambao umedorora katika miaka ya karibuni. Shirika la habari la Reuters wiki iliyopita lilisema kuwa Lammy anatarajiwa kukutana na maafisa wa China mjini Beijing, pamoja na wawakilishi wa makampuni ya Uingereza mjini Shanghai, na kwamba ziara hiyo itakuwa ya siku mbili kulingana na vyanzo vya kuaminika.

Msemaji wa ofisi ya masuala ya Kigeni na Jumuia ya Madola ya Uingereza ameambia VOA kwamba ziara ya Lammy haijatangazwa kwa umma. Wakati wa kampeni za bunge mwaka huu, chama cha Labour cha Uingereza kiliahidi kutathmini upya, uhusiano wa China na Uingereza ili kujenga ushirikiano wa muda mrefu.

Wakati wa mawasiliano ya simu ya Agosti, kiongozi wa China Xi Jingping na Waziri Mkuu wa Uingereza Kier Stammer walisema kuwa licha ya tofauti zilizopo, kuna haja ya kuwa na mashauriano ya dhati, wakati wakiahidi kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kimataifa.

Forum

XS
SM
MD
LG