Seneta mzawa huko Australia alimwambia Mfalme Charles III kwamba Australia sio ardhi yake na Waziri Mkuu Anthony Albanese alisema mfalme hahitajiki kama mkuu wa nchi wakati mfalme wa Uingereza alipolitembelea bunge la Australia leo Jumatatu.
Seneta huyo mzawa Lidia Thorpe aliondolewa sehemu ya mapokezi ya bunge kwa wanandoa wa kifalme baada ya kupiga kelele kwamba wakoloni wa Uingereza wamechukua ardhi na mifupa ya wazawa. “Mlifanya mauaji ya kimbari dhidi ya watu wetu” alisema.
“Tupe kile mlichotuibia, mifupa yetu, mafuvu yetu, watoto wetu, watu wetu. Mmeiharibu nchi yetu. Tupeni mkataba. Tunahitaji mkataba.”
Mfalme Charles alizungumza kwa sauti ya chini na Waziri Mkuu Anthony Albanese wakati maafisa wa usalama wakimzuia Seneta Thorpe kuwakaribia.
Forum