Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, uchaguzi huo huenda ukawa na ushindani mkali kulingana na wachambuzi ingawa upinzani uliogawanyika unatoa nafasi kubwa kwa chama cha Masisi cha Botswana Democratic Party, BDP, ambacho kimetawala taifa hilo la watu milioni 2.3 tangu kujipatia uhuru wake kutoka kwa Uingereza maka 1966.
Botswana imekuwa na ustawi na udhabiti kwa muda mrefu, ziadi kutokana na utajiri wa Almasi, pamoja na idadi ndogo ya watu ambao hupewa huduma za bure za elimu na afya. Hata hivyo kushuka kwa bei ya Almasi kwenye soko la kimataifa katika miaka ya karibuni kumepelekea kushuka kwa mapato ya ndani, wakati taifa likijirahidi kuwekeza kwenye sekta nyingine.
Wapinzani wanasema kuwa chama cha BDP, kimebaki madarakani kwa muda mrefu zaidi na kwa hivyo kulaumiwa kuvuruga uchumi pamoja na ufisadi, madai ambayo kimekanusha. Wakati wa mdahalo uliofanyika wiki iliopita, Masisi alisema kuwa ni kweli Almasi hazijakuwa zikinunuliwa tangu Aprili, na kwamba uchumi umeshuka, lakini mfumo wa kiuchumi ungali dhabiti.