Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 09:56

Botwana yadaiwa kutowapa fursa wanawake kushiriki katika jukwaa la kisiasa


Mwanamke akipiga kura huko Botwana Picha na ALEXANDER JOE / AFP
Mwanamke akipiga kura huko Botwana Picha na ALEXANDER JOE / AFP

Vyama vya siasa vimekamilisha orodha yao ya wagombea wao wa uchaguzi mkuu wa 2024 uliopangwa kufanyika Oktoba na wagombea wengi ni wanaume.

Katika chama tawala cha Botswana Democratic Party (BDP), kati ya wagombea 200 wa ubunge, ni 20 pekee ni wanawake.

Mwanaharakati wa masuala ya jinsia Pamela Dube aliiambia Sauti ya Amerika kuwa hali hiyo inatia wasiwasi hasa ikizingatiwa ni wanawake wachache waliochaguliwa mwaka 2019.

“Hali ya mambo katika ushiriki wa wanawake kisiasa nchini Botswana inasikitisha. Wakati takwimu, zinaonyesha wanawake ni zaidi ya asilimia 50 ya wapiga kura,” alisema Dube.

Na aliongeza kuwa “uwakilishi wa wanawake katika nafasi za kuchaguliwa bado ni mdogo sana. Nina wasiwasi mkubwa kama tutaona mabadiliko katika uchaguzi ujao wa Oktoba.”

Botswana ina mapungufu katika mfumo ulioanzishwa na jumuiya ya kikanda ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika-SADC katika kufanikisha kufikia usawa wa kijinsia. Sera ya jumuiya hiyo inatetea uwakilishi sawa katika nafasi za siasa na za kufanya maamuzi.

Wafuasi wa chama cha Botswana Congress Party (BCP) wakicheza na kushangilia wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi za mgombea urais Dumelang Saleshando.
Wafuasi wa chama cha Botswana Congress Party (BCP) wakicheza na kushangilia wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi za mgombea urais Dumelang Saleshando.

Dube anasema chama tawala cha BDP kinapaswa kuweka mgao wa kijinsia ili kusukuma kutengwa kwa mgao wa viti. upendeleo wa kijinsia ili kushinikiza kutenga viti katika bunge.

“Botswana haina sheria kama hizo, au hata vipengele vya katiba. Inasikitisha hata kwamba tathmini ya mswaada uliopo kwenye bunge uko kimya kuhusiana na suala hili.” Alisema Dube.

Msemaji wa muungano wa upinzani wa Umbrella for Democratic Change (UDC), Moeti Mohwasa, anasema sheria za uchaguzi nchini humo haziwapendelei wanawake.

Botswana inatumia mfumo wa zamani kutoka mwanzo hadi mwisho, ambapo wapiga kura wanachagua mgombea mmoja, hatua inayopingwa na upinzani.

Rais wa Botswana, Mokgweetsi Masisi alipokuwa akihutubia baada ya kuapishwa. Picha na Monirul Bhuiyan / AFP.
Rais wa Botswana, Mokgweetsi Masisi alipokuwa akihutubia baada ya kuapishwa. Picha na Monirul Bhuiyan / AFP.

Mohwasa alisema “Huwezi kutarajia mfumo huo huo au hali ambayo ni mfumo dume, wa kiconservative kuwaruhusu wanawake kupande na kushikilia nafasi za mamlaka.”

“Msimamo wetu ni kwamba unahitaji kuwa na mfumo mchanganyiko, ambao utakuwa ni wa sasa na wazamani na pia kuorodhesha mfumo wenyewe. Kama ukiziangalia nchi ambazo zina mifumo inayohusu orodha, utagundua kwamba wanawake wanawezeshwa zaidi.” aliongeza.

Afisa wa Program ya Wanawake katika Ushiriki wa Kisiasa (WPP) yenye makao yake Maputo, Sifisosami Dube anasema Botswana inapaswa kurekebisha sheria zake za uchaguzi chini ya mchakato wa hivi karibuni wa mapitio ya katiba.

“Kuna haja ya kuwashika mkono wanawake katika uongozi wa kisiasa kutoka wakati wanapofanya kampeni, au wakati wanapofikiria kuhusu kampeni mpaka wakati watakapoingia katicha uchaguzi na wakati wanapokuwa katika uongozi wa kisiasa. Kwasababu mara wanapokuwa katika ofisi za kisiasa, kuna hali isiyo ya kawaida huko; wanahitaji kutiwa moyo wakati wote.” alisema afisa huyo wa Program hiyo ya Wanawake ya WPP.

Wakati Botswana inapambana kuwapata wanawake wengi kuingia katika siasa, nchi kama Tanzania, Angola, Msumbiji, Namibia, Afrika Kusini, na Zimbabwe zina uwakilishi wa wanawake zaidi ya asilimia 30 katika mabaraza ya bunge.

Forum

XS
SM
MD
LG