Blinken akutana na Marais wa Nigeria na Ivory Coast

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alipowasili katika makao makuu ya AfricaRice huko Abidjan on Januari 23, 2024. Picha na AFP

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken anakutana na Marais wa Nigeria na Ivory Coast katika jitihada za kuunda mshikamano na mataifa hayo mawili muhimu ya kidemokrasia barani Afrika wakati mizozo ikiikumba dunia.

Mjini Abidjan, Blinken alikutana na Rais wa Ivory Coast, Alassane Ouattara, kiongozi mkongwe ambaye amepata sifa za Marekani kwa kuimarisha demokrasia, kabla ya kuelekea Abuja kumuona Rais wa Nigeria Bola Tinubu, aliyechaguliwa mwaka jana .

Blinken, wakati wa mkutano na waandishi wa habari na Rais Ouattara, aliipongeza Ivory Coast kwa uongozi wake katika kukabiliana na itikadi kali na ghasia.

“Tunashukuru sana uongozi ulioonyeshwa na Cote d'Ivoire kukabiliana na itikadi kali na vurugu. Tunatangaza dola bilioni 45 za ufadhili mpya, kupitia mpango wa usalama wa Marekani wa kuzuia migogoro na kukuza utulivu kwa mataifa ya pwani ya Afrika Magharibi.”Alisema Waziri huyo wa wa Mambo ya Nje wa Marekani

“Kwa uwekezaji huu mpya, Marekani itakuwa imewekeza karibu dola bilioni 300 katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, usaidizi unaolenga utulivu katika pwani ya Afrika Magharibi,” aliongeza.

Blinken yuko katika ziara ya mataifa manne, akinadi kwamba Marekani ni mshirika mkuu wa kiuchumi na usalama wa bara hilo wakati wa mizozo ya kikanda na kimataifa.