Biden kuziondolea marufuku nchi nane za Kusini mwa Afrika

Rais wa Marekani Joe Biden

Ikulu ya Marekani imesema utawala wa Rais Joe Biden utaondoa marufuku katika nchi nane za Kusini mwa Afrika yaliyokuwa yamewekwa mwezi uliopita kuhofia maambukizi ya haraka ya kirusi cha Omicron kinachosababisha COVID 19.

Raia wa kigeni waliokuwa wamezuiwa kuingia Marekani kwa sababu wapo katika mojawapo ya nchi nane ndani ya siku 14 zilizopita wataruhusiwa tena kuingia nchini Marekani.

Pia kwa safari za ndege zinazoondoka baada ya saa sita usiku kwa saa za Marekani, afisa mwandamizi amesema, imethibitisha ripoti ya awali ya shirika la habari la roita.

Novemba 29 Marekani iliwazuia takriban watu wote wasiokuwa raia wa Marekani ambao karibuni walikuwepo Afrika Kusini, Botswana, Zimbabwe, Namibia, Lesotho, Eswatini, Msumbiji na Malawi, ikichukua tahadhari kutokana na kirusi kilichogulnduiwa afrika ya kusini kwa mara ya kwanza.

Katika mtandao wa Twitter Biden aliandika : "Tutaondoa masharti katika nchi za kusini mwa afrika kuanzia desemba 30."

Amesema uamuzi huo umependekezwa na vituo vya kudhibiti na kuziya magonjwa –CDC.

\