Biden atajaribu kuonyesha kwamba katika masuala makubwa ya kimataifa, Washington ni mshirika bora kuliko Beijing au Moscow, na kwamba G20 inasalia kuwa jukwaa muhimu, AFP iliripoti Alhamisi.
Lakini mgawanyiko mkubwa kuhusu vita vya Russia nchini Ukraine na jinsi ya kusaidia mataifa yanayoibukia kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, unatarajiwa kutatiza makubaliano wakati wa mkutano wa siku mbili mjini New Delhi.
Biden pia atazuru Vietnam siku ya Jumapili ambapo anatarajiwa kuimarisha uhusiano na hasimu huyo wa zamani wa Marekani, katika jitihada zaidi za kukabiliana na ushawishi wa China unaoongezeka.
Ndege ya rais, Air Force One, iliondoka Joint Base Andrews karibu na Washington na inatarajiwa kuwasili India siku ya Ijumaa.