Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 10:58

Umoja wa Afrika kuwa mwanachama kamili wa G-20


Wanafunzi wakikamilisha michoro ya rais wa Marekani Joe Biden katika shule ya sanaa huko Mumbai, Septemba 7 2023. Picha na INDRANIL MUKHERJEE / AFP.
Wanafunzi wakikamilisha michoro ya rais wa Marekani Joe Biden katika shule ya sanaa huko Mumbai, Septemba 7 2023. Picha na INDRANIL MUKHERJEE / AFP.

Kundi la G-20, linalojumuisha nchi tajiri na zenye nguvu duniani, litatoa uanachama kwa Umoja wa Afrika, vyanzo vilisema Alhamisi.

Hatua hiyo itaipa Umoja wa Afrika kuwa na chombo hicho cha bara la Afrika lenye nchi wanachama 55, hadhi sawa na Umoja wa Ulaya –ambao kwa sasa ni kambi pekee ya kikanda yenye unachama kamili – na kuufanya Umoja wa Afrika kubadilisha hadhi yake ya sasa ya "taasisi ya kimataifa iliyokaribishwa".

Afisa wa AU aliliambia Shirika la habari la Reuters kwamba kundi hilo litakuwa mwanachama wa kudumu. Afisa huyo hakutaka jina lake litajwe kwa vile hana mamlaka ya kuzungumzia suala hilo.

Wachambuzi wanasema kwamba wakati kikao cha G20 kitakapoanza Jumamosi mjini New Dehli, kutokuwepo kwa rais wa China Xi Jinping huenda kukagubika juhudi za kushughulikia masuala muhimu ya kimataifa kama vile mabadiliko ya hali ya hewa na vita vya Russia nchini Ukraine.

Beijing haikusema sana kiongozi huyo hatahudhuria.

Katika taarifa ya sentensi moja kwenye tovuti yake Jumatatu, Wizara ya Mambo ya Nje ya China ilitangaza kwamba Waziri Mkuu Li Qiang atamwakilisha rais wa China. Katika mkutano na waandishi wa habari baadaye siku hiyo, msemaji wa wizara hiyo Mao Ning hakuwa na la kuongeza, zaidi ya kusema, "China kwa muda wote imekuwa ikizingatia umuhimu mkubwa wa umoja huo na itashiriki kikamilifu katika matukio ya G20."

Wachambuzi wanasema kuwa uamuzi wa Xi wa kutohudhuria mkutano huo unazua maswali na kuangazia kipaumbele cha mabadiliko ya ajenda ya sera ya mambo ya nje ya Beijing. Kwa kuanzia wanasema, kutohudhuria kunaamanisha kukosa fursa za kushirikiana na viongozi wengine wa ngazi za juu duniani na kuboresha mahusiano.

Baadhi ya taarifa hii inatoka shirika la habari la Reuters

Forum

XS
SM
MD
LG