Benki ilikanusha madai hayo na kampuni ya ujenzi ya Uturuki Yapi Markezi haikuweza kupatikana kutoa maoni.
Serikali ya rais Samia Suluhu Hassan, ambayo inakamilisha miradi mikubwa ya usafiri iliyoanzishwa na aliyekuwa rais wa nchi hiyo marehemu John Magufuli, amekuwa akichukua hatua kwa baadhi ya mikataba iliyopitishwa ambayo inatuhumiwa kura rushwa.
Rais Samia Suluhu aliivunja bodi ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) siku ya Jumapili bila kutaja sababu maalum zaidi ya kuamuru hatua za kisheri zichukuliwe dhidi mtu yeyote atakayebainika kuhusika na matumizi mabaya ya fedha za umma.
Katika ripoti ya ukaguzi ya kila mwaka ambayo shirika la habari la Reuters imeiona siku ya Alhamisi, Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Charles Kichere alisema kuwa Standard Chartered, ambayo ilikuwa ikitoa mikopo kwa ajili ya miradi ya serikali, imekubali kuhusika kuipa zabuni kampuni ya ukandarasi ya Yapi.
"Standard Chartered Bank ... ilitoa masharti ambayo yangefanya ikubali kuwa mratibu wa kimataifa na wakala anayeongoza kutoa misaada na mikopo kwa wizara ya fedha na mipango endapo tu kampuni ya Yapi Markezi ingechaguliwa kuwa mkandarasi," mkaguzi huyo alisema.
Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la Reuters