Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 22:08
VOA Direct Packages

Wataalam wa Tanzania waomba waziri mkuu na baraza la mawaziri kuwajibishwa kwa kushindwa kulinda rasilimali za nchi


CAG akimkabidhi ripoti Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
CAG akimkabidhi ripoti Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Baadhi ya wachambuzi na wasomi wameitaka serikali ya Tanzania kumuwajibisha waziri mkuu na baraza la mawaziri kufuatia kushindwa kusimamia rasilimali za nchi baada ya kuwepo kwa upotevu mkubwa wa pesa unaoendelea kujitokeza.

Hali hiyo imendelea kujitokeza kwa miaka miwili ndani ya serikali ya awamu ya sita, huku wananchi wakitakiwa kuacha kunung’unika na badala yake kudai uwajibikaji kwa viongozi. Wachambuzi hao wamesema hatua iliyochukuliwa na serikali kufuatia ripoti ya CAG sio mwarubaini wa kumaliza ubadhirifu unaoendelea kufanywa na baadhi ya watendaji wa serikali. Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya kuvunjwa kwa bodi ya wakurugenzi wa shirika la reli Tanzania (TRC) na kutengua uteuzi wa mtendaji mkuu wa wakala wa ndege za serikali.

Professa Xavery Lwaitama muhadhiri msitaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam amesema Rais anapaswa kuonyesha mfano kwa watendaji wengine kwa kumuondoa madarakani waziri mkuu na kuvunja baraza la mawaziri kwa kuwa wameshindwa kusimamia wizara hizo kwa miaka miwili ambayo imeonekana kuna upotevu mkubwa wa pesa pia hatua hiyo itarudisha imani kwa wananchi na kuonyesha hasira ya serikali. Mchambuzi wa kisiasa na kijamii kutoka chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Dkt Paul Loisulie,amewataka wananchi kudai uwajibikaji wa rasilimali za nchi ili kusaidia kuwepo kwa sauti moja itakayo wafanya viongozi kuchukua hatua na kulinda rasilimali za nchi kuliko kunung’unika.

Amri Ramadhani Sauti ya Amerika Dar es Salaam

XS
SM
MD
LG