Baadhi ya maafisa wa polisi wa London wagoma kubeba silaha baada ya mwenzao kushtakiwa kwa mauaji

Polisi nchini Uingereza.

Baadhi ya maafisa wa polisi wa London wamekataa kubeba silaha baada ya mwenzao kushitakiwa kwa mauaji katika tukio la ufyatuaji risasi kwa  mtu mmoja mweusi ambaye hakuwa na silaha.

Shitaka hilo dhidi ya afisa polisi ni la nadra sana kutokea uingereza.

Gazeti la telegraph limeripoti kwamba maafisa wa polisi 300 takriban asilimia 10 ya polisi walio na silaha wamekataa kubeba silaha zao kufuatia mashitaka dhidi ya polisi mwenzao.

Hatua hiyo ya maafisa wa polisi imepelekea makao makuu ya jeshi la polisi kuiomba wizara ya ulinzi kusaidia kuhusu sera ya kupambana na ugaidi.

Wizara ya Ulinzi itawapa London wanajeshi ambao watafanya kazi maalum lakini si kazi za kawaida za polisi.

takriban polisi mmoja kati ya kumi mjini London anabeba silaha baada ya kupata mafunzo ya kina.

Chris Kaba mwenye umri wa miaka 23 ni mtu mweusi aliyeuwawa katika mapambano na polisi mwaka jana. Shirika la habari la AP linaripoti kwamba Kaba alipigwa risasi moja wakati akiwa amekaa kwenye gari lake.