Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 22:23

Maafisa 1,000 wa polisi wa mji wa London wasimamishwa kazi kwa utovu wa nidhamu


Maafisa wa polisi wakilinda usalama karibu na jengo la Bunge mjini kati London, Machi 23, 2017, siku moja baada ya shambulio la kigaidi.
Maafisa wa polisi wakilinda usalama karibu na jengo la Bunge mjini kati London, Machi 23, 2017, siku moja baada ya shambulio la kigaidi.

Takriban maafisa 1,000 wa polisi wamesimamishwa kazi au kuwekewa masharti ya kazi ikiwa ni sehemu ya juhudi za kulisafisha jeshi la polisi la mji mkuu wa London lililokabiliwa na kashfa, mkuu wa polisi amesema Jumanne.

Kikosi hicho kikubwa nchini humo kimekabiliwa na msururu wa kashfa ambazo zimedhoofisha imani kwa polisi wa Uingereza.

Kashfa hizo zinajumuisha ubakaji na mauaji ya msichana aliyenyakuliwa kimabavu barabarani na afisa mmoja wa polisi.

Kulingana na polisi, kati ya maafisa 34,000, 201 wamesimamishwa kazi kwa sasa, na takriban 860 hawaruhusiwi kufanya baadhi ya shughuli.

Forum

XS
SM
MD
LG