Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 16:08

Wizara ya Ulinzi Uingereza: Makamanda watatu wa Kikosi cha anga cha Russia wamejiuzulu au kuuwawa


Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak alipotembelea Chuo Kikuu cha Writtle karibu na Chelmsford Septemba 21, 2023. AFP
Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak alipotembelea Chuo Kikuu cha Writtle karibu na Chelmsford Septemba 21, 2023. AFP

Kwanza Kanali Konstantin Zizevsky, amanda wa kikosi aliuawa karibu na mwanzo wa uvamizi wa Russia.  Kisha, Kanali Vasily Popov huenda aliuawa katika eneo la  Orikhiv lenye upinzani mkubwa, mapema mwezi huu, kwa mujibu wa  ripoti hiyo ya kijasusi.

Uzoefu wa mojawapo ya vikosi vya hali ya juu vya anga vya Russia unaonyesha viwango vya ushujaa mkubwa na matumizi makubwa katika jeshi la nchi hiyo , pamoja na safu zake za juu, wizara ya Ulinzi ya Uingereza ilisema Jumamosi katika taarifa yake ya kila siku ya kijasusi juu ya uvamizi wa Russia huko Ukraine

Makamanda watatu waliofuatana wa Kikosi cha 247 cha anga wamejiuzulu au kuuwawa, ilisemekana. Kwanza, Kanali Konstantin Zizevsky, amanda wa kikosi aliuawa karibu na mwanzo wa uvamizi wa Russia. Kisha, Kanali Vasily Popov huenda aliuawa katika eneo la Orikhiv lenye upinzani mkubwa, mapema mwezi huu, kwa mujibu wa ripoti hiyo ya kijasusi.

Wakati huo huo, Kanali Pytor Popov huenda alijiuzulu uongozi mwezi Agosti, ripoti hiyo ilisema, baada ya kupinga kushindwa kwa jeshi kuirejesha miili ya majeruhi wa Russia.

Forum

XS
SM
MD
LG