Rais Zuma akifuatana na viongozi wengine watatu wa Afrika walikutana na Bw Gadhafi nyumbani kwake Tripoli Jumapili kwa masaa kadhaa kujadili mpango wa kusitisha mapigano nchini Libya.
Masharti ya mpango huo hayajajulikana baado, lakini viongozi wa upinzani wa Libya wamesema hawatakubaliana na chechote kile isipokuwa kuondolewa kwa utawala wa Ghadafi, huku maafisa wa Libya wakisema hatondoka madarakani.
Mpango huo wa AU unataka pia kusitishwa kwa mashambulio ya anga ya NATO dhidi ya majeshi ya serikali ili kuupatia nafasi mpango wa kusitisha mapigano kufanikiwa.
Rais wa Afrika Kusini ambae anafuatana na marais wa Mauritani, Mali na Congo pamoja na mjumbe kutoka Uganda, anatazamiwa kusafiri hadi Benghazi, ngome ya upinzani, Jumatatu kwa mazungumzo na viongozi wa upinzani juu ya mpango wao.
Wakati huo huo, mashmabulio ya ndege ya NATO yamerudisha nyuma majeshi ya serikali kutoka mji muhimu wa mashariki wa Ajdabiya Jumapili na kuwaruhusu wapiganaji wa upinzani kuuchukua tena mji huo.