Naibu katibu mkuu wa chama hicho Nomvula Mokonyane, ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba "hatutakwenda vitani tukiwa na dhana ya kushindwa," aliongeza kusema "tuko vitani ili kupata ushindi."
Waafrika Kusini wanatarajiwa kupiga kura tarehe 29 Mei, ili kulichagua bunge ambalo hapo tena limamteuwa rais mpya.
Uchunguzi wa maoni unaonesha kwamba chama cha ANC kinaweza kupoteza wingi wake kwenye bunge kutokana na matatizo ya ulajirushwa, hali mbaya ya uchumi, ukosefu wa ajira na kashfa za mara kwa mara dhidi ya maafisa wa chama tawala cha ANC.
Chama kikuu cha upinzani Demokratik party kimeungana na vyama vingine vidogo katika juhudi za kukishinda chama cha ANC kwenye uchaguzi huo.