Amnesty International yaviasa vikosi vya usalama vya Israeli na wanamgambo wa Palestina kulinda uhai wa raia

Moshi mkubwa ukiwa umetanda katika anga ya Mji wa Gaza wakati wa shambulizi la anga la Israel Oktoba 9, 2023. Picha na MAHMUD HAMS / AFP.

Vikosi vya usalama vya Israeli na makundi ya wanamgambo wa Palestina ni lazima wafanye kila juhudi kulinda uhai wa raia katika vita vilivyozuka hivi leo huko Israeli na katika maeneo ya Palestina yanayokaliwa kimabavu, imesema Amnesty International wakati idadi ya vifo vya raia ikiongezeka.

Kusambaa kwa vita hivi leo kulianza kwa Hamas kushambulia kwa roketi ndani ya Israeli na kuanzisha operesheni iliyokuwa haijawahi kushuhudiwa iliyofanywa na wapiganaji wake huko kusini mwa Israeli.

“Sisi tumeshtushwa sana na ongezeko la idadi ya vifo vya raia huko Gaza, Israel na maeneo yanayokaliwa kimabavu Ukingo wa Magharibi na tunatoa wito wa haraka kwa pande zote katika mgogoro huu kuheshimu sheria za kimataifa na kufanya kila juhudi kuepusha umwagaji damu zaidi wa raia.

Chini ya sheria za kimataifa za binadamu pande zote katika mgogoro wanajukumu la dhahiri kulinda maisha ya raia ambao wako katika eneo la mapigano,” alisema Katibu Mkuu wa Amnesty International, Agnes Callamard.

“Kitendo cha kuwalenga raia kwa makusudi, na kufanya mashambulizi yasiyolingana, na mashambulizi holela ambayo yanaua na kujeruhi raia ni uhalifu wa kivita. Israeli ina rekodi ya kutenda uhalifu wa kivita bila ya kuwajibishwa katika vita vya awali huko Gaza.

Vikundi vya Wapalestins vyenye silaha kutoka Gaza, ni lazima vijizuie kuwalenga raia na kutumia silaha kiholela, kama walivyokuwa wakifanya huko nyuma, na kwa nguvu zaidi katika tukio hili, vitendo vinavyopelekea uhalifu wa kivita.”

Hatua ya Israeli kulipiza kisasi huko Gaza imeuwa watu wasiopungua 232 na kujeruhi takriban watu 1,700, kulingana na Wizara ya Afya ya Palestina.

Vyombo vya habari vya Israeli vimeripoti kuwa watu wasiopungua 250 wamefariki na wizara ya afya ya Israeli imeripoti kuwa zaidi ya watu 1,500 wamejuruhiwa katika shambulizi lililofanywa na vikundi venye silaha vya Wapalestina.

Jeshi la Israeli limethibitisha kwa vyombo vya habari kuwa raia wa Israeli, pamoja na wanajeshi wametekwa na vikundi venye silaha vya Wapalestina na kuwa mateka.

Ukamataji wa raia na kuwateka kumepigwa marufuku na sheria za kimataifa na kunawezaz kupelekea uhalifu wa kivita.

Raia wote waliotekwa ni lazima waachiliwe mara moja, bila masharti, na bila kudhuriwa.

Wote ambao wametekwa lazima wafanyiwe ubinadamu, kulingana na sheria ya kimataifa na wapewe matibabu.

Chanzo cha habari hii ni Shirika la Amnesty International.