Baada ya kula kiapu, Deby aliwahutubia viongozi saba kutoka mataifa ya Afrika Magharibi na wageni wa heshima pamoja na wananchi wa Chad.
Alitoa wito kwa Wachad wote waliompigia kura na wapinzani wake kufanyakazi nae na kwamba ataheshimu uwamuzi wao ambao ni muhimu kiatika kuendeleaza demokrasia nchini mwao.
Deby alipata asilimia 61 za kura katika uchaguzi uliofsnyika Mei 6 ambapo mashirika yasiyo ya kiserikali yalisema haukuwa wa kuaminika wala huru na ambapo mpinzani wake kuu aliuita uchaguzi huo kuwa uliokuwa na udanganyifu.
Sherehe hizo za kuapishwa kwa kiongozi huyo kunafikisha kikomo cha miaka mitatu ya utawala wa kijeshi katika nchi ambayo inapambana na wapiganaji mbali mbali ndani ya nchi na ukanda wa Sahel huko Africa Magharibi.