Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 08:57

Jenerali Mahamat Idriss Deby ameshinda uchaguzi wa rais nchini Chad


Mahamat Idriss Deby Itno ameshinda uchaguzi wa urais nchini Chad. April 14, 2024.
Mahamat Idriss Deby Itno ameshinda uchaguzi wa urais nchini Chad. April 14, 2024.

Baraza la Katiba lililotangaza ushindi huo pia lilikataa ombi lililotolewa na Waziri Mkuu Succes Masra la kutaka kufutwa matokeo hayo.

Kiongozi wa kijeshi wa Chad, Jenerali Mahamat Idriss Deby Itno ameshinda uchaguzi wa rais wa nchi hiyo wa Mei 6 kwa asilimia 61 ya kura, kulingana na matokeo ya mwisho yaliyotangazwa Alhamisi.

Baraza la Katiba, ambalo lilimtangaza mshindi, pia lilikataa ombi lililotolewa na Waziri Mkuu, Succes Masra la kufuta matokeo. Masra ambaye alidai ushindi, alisema katika ujumbe wa mitandao ya kijamii kwamba hakubaliani na matokeo hayo, lakini akaongeza “hakuna njia nyingine ya kisheria ya kitaifa”. Alitoa wito kwa wafuasi wake “kuendelea kudai haki” lakini kwa amani.

Jenerali Mahamat Idriss Deby Itno akipiga kura yake ya urais Mei 6 mjini N'djamena.
Jenerali Mahamat Idriss Deby Itno akipiga kura yake ya urais Mei 6 mjini N'djamena.

Deby ameuita uchaguzi huo ni kumaliza miaka mitatu ya utawala wa kijeshi katika nchi muhimu katika mapambano dhidi ya jihadi kwenye eneo tete la Sahel barani Afrika.

Utawala huo kwa muda mrefu umekuwa ukiwakandamiza viongozi wa upinzani, vile vile na mpinzani mkuu wa Deby aliuawa mwezi Februari.

Forum

XS
SM
MD
LG