Masra, ambaye ni mpinzani mkuu wa utawala wa kijeshi ulioingia madarakani Aprili 2021, aliteuliwa kuwa waziri mkuu katika serikali ya mpito mnamo mwezi Januari, miezi minne kabla ya uchaguzi mkuu, katika hatua iliyoonekana kama ya kuwafurahisha wanasiasa wa upinzani.
Aliidhinishwa kugombea urais mnamo mwezi March, katika uchaguzi unaolenga kuirudisha nchi hiyo katika utawala wa kikatiba, taifa hilo la Afrika Magharibi linalozalisha mafuta na ni miongoni mwa nchi katika ukanda wa Sahel, ambazo zimekumbwa na mapinduzi ya kijeshi.
Kabla ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa rasmi, Masra alikuwa amejitangazia ushindi akidai kwamba kulikuwa na udanganyifu katika hesabu ya kura.
Tume ya uchaguzi ya Chad imesema kwamba Deby ameibuka mshindi kwa kupata asilimia 61 na ushindi wake umeidhinishwa na baraza la kikatiba.
Masra amekubali uamuzi wa baraza la katiba na kusema kwamba hakuna njia nyingine za kisheria anaweza kutumia kupinga matokeo hayo.
Forum