AFCON 2019 : Senegal yatinga robo fainali za raundi ya pili

AFCON 2019 : Ratiba ya Raundi ya 16

Timu ya taifa ya Senegal “Simba wa Teranga” wamefanikiwa kuingia robo fainali za michuano ya kombe la mataifa ya Afrika – Afcon inayoendelea mjini Cairo, Misri.

Senegal imefanikiwa kuishinda Uganda Cranes kwa bao 1-0 katika mchezo wa raundi ya pili uliofanyika kwenye uwanja wa kimataifa wa soka wa Cairo.

Mchezo huo ambao ulipoanza ulitawaliwa na kadi za njano kwa upande wa wachezaji wa Uganda ambao ni pamoja na nahodha wa timu hiyo goli kipa Dennis Onyango alijikuta akipata kadi hiyo alipofanya madhambi wakati akitoka kuokoa hatari langoni mwake.

Sadio Mane

Mchezaji wa kimataifa wa Senegal anayecheza katika ligi ya Uingereza Sadio Mane aliyetumia nafasi ya makosa ya walinzi wa Uganda na kupachika bao katika dakika ya 15 ya mchezo huo.

Katika kipindi cha pili Uganda ilifanya mabadiliko kwa kumtoa mshambuliaji Patrick Kadu na kumwingiza Allan Kyambadde. Lakini bado hawakufanikiwa kupata bao la kusawazisha kutokana na makosa katika safu yao ya ushambuliaji.

Katika dakika ya 14 Sadio Mane aliangushwa katika eneo la hatari na golikipa Dennis Onyango ambapo Mane alichukua fursa ya kupiga penalti hiyo na Dennis Onyango akaidaka penalti yake na kuamsha shangwe kwenye jukwaa la washangiliaji wa Uganda.

Emmanuel Okwi

Dakika ya 18 Uganda walifanya shambulizi na kusababisha kupata kona ambayo katika purukushani mshambuliaji Emmanuel Okwi alitaka kufunga bao lakini aligongana na kipa wa Senegal Edouard Mendy anayecheza soka la kulipwa nchini Ufaransa.

Katika dakika ya 20 ya kipindi cha pili hali ingeweza kuwa mbaya zaidi kwa Uganda lakini ukuta wa Uganda ulifanya kazi ya ziada kwa kupangua shambulizi la Senegal. Mchezaji Bevis Mugabi alifanya kazi ya ziada kuokoa mashambulizi na kutoa kona.

Krepin Diata

Dakika ya 24 Senegal walifanya mabadiliko na kumwingiza mchezajihatari wa kiungo Krepin Diata ambaye anakumbukwa kwa kuizamisha timuya Tanzania kwenye michuano hiyo anayechezea klabu ya Bragge huko Ubelgiji.

Yusuf Sarali anayechezea timu ya Tubsui Bordaux Ufaransa aliisumbua sana ngome ya Uganda

Na hatimaye Ugandawalifanya tena mabadiliko kwakumtoa khalid Aucho na kuingizwa Allan Katerega mchezaji wa Marisburg United ya Afrika Kusini lakini hali bado ilikuw angumu kwaUganda waliojitahidi kudhibiti sehemu ya kati.

Dakika ya 33 Okwi aliangushwa nje kidogo ya eneo la hatari la Senegal, lakini Katerega alipiga kiki ya hatari iliyookolewa na mlinzi wa lango la Senegal.

Senegal wafanya mabadiliko

Senegal walifanya mabadiliko mengine kwa kumwingiza Keita Balde na kumtoa Alfred Ndiaye kuongeza nguvu upande wa kiungo. Huku kikosi cha ushangiliaji cha nchi kikiendelea kuwapa nguvu wachezaji kwani kilikuwa hakichoki kushangilia wakati wote wa mchezo huo.

Senegal ilifanya tena mabadiliko kwa kumuingiza Mbaye Diagne kuchukua nafasi ya Mbaye Niang. Na kunako dakika ya 40 Sadio Mane alikosa nafasi ya wazibaada ya walinzi wa Uganda kuokoa mpira alipokuwa akienda kumwona kipa Dennis Onyango.

Pamoja na kupoteza mchezo huo Uganda imeonyesha uwezo katika timu za Afrika mashariki baada ya kumaliza kwa kufanikiwa kufika raundi ya pili na kupambana vilivyo na timu kubwa za Afrika za Misri na Senegal licha ya kupoteza michezo hiyo.

Baada ya mechi hiyo mchezaji mahiri wa Senegal na Mabingwa wa kombe la UEFA Liverpool Sadio Mane ambaye mpaka sasa anaongoza kwa kufunga mabao 3, aliwasifu Uganda Craneskwamba ni timu yenye kutumia nguvu na yenye uwezo.

Alipoulizwa kuhusu kukosa penati kwa mara ya pili, alisema wakati mwingine atamwachia mtu mwingine apige penati huku akicheka.

Nini walichosema Uganda

Naye mchezaji machachari wa timu ya taifa ya Uganda Cranes na Simba ya Tanzania Emmanuel Okwi alikiri kwamba Senegal ni timu ngumu na wamejitahidi kwa kadri ya uwezo wao kupambana nao na pia kuwashukuru kwa dhati raia wa Uganda na Afrika mashariki kwa ujumla kwa kuwaunga mkono kwenye mchezo uliopelekea timu hiyi kufungasha virago.

Senegal sasa itakutana na timu ngumu ya Benin siku ya Julai 10 katika robo fainali itakayofanyika kwenye uwanja wa June 30. Timu ya Benin imeshangaza wengi baada ya kuwang’oa vigogo wa soka barani Afrika Morocco kwa jumla ya penati 4-1 baada ya kutoka sare bao 1-1 katika muda wa dakika 90 na baadaye dakika 30 za nyongeza.

Benin imeweka historia katika nchi yao wakishiriki kwa mara ya nne na kuingia robo fainali kwa mara ya kwanza katika michuano hiyo.