Shirika la ndege la Delta linaendelea kuhangaika kurejesha safari zake, siku ya tatu baada ya hitilafu ya mtandao duniani iliyo sumbua safari za ndege sehemu mbalimbali duniani na kusababisha maelfu ya wasafiri kukwama.
Shirika hilo la ndege lenye ofisi zake Atlanta limekatisha safari za ndege 778, au takribani asilimia 20, mpaka kufikia saa saba na nusu mchana wa Jumatatu, kwa mujibu wa FlightAware. Inaakuwa nusu ya jumla ya safari zilizo katishwa.
Waziri wa usafiri wa Marekani, Pete Buttigieg alisema Jumapili, ofisi yake imepokea mamia ya malalamiko kuhusiana na kitengo cha huduma za wateja cha Delta na watu wakitaka kurudishiwa pesa zao haraka.