Mamluki wa kundi la Wagner wamesema mwezi uliopita kuwa wapiganaji wake na wanajeshi wa Mali wamepata hasara katika mapigano makali dhidi ya waasi wa Tuareg na wapiganaji wa kiislamu washirika wa al Qaeda karibu na mpaka wa Mali na Algeria.
Waasi wa Tuareg upande wa kaskazini mwa Mali wamesema wamewauwa Warussia takribani 84 wa kundi la mamluki la Wagner na wanajeshi 47 wa Mali katika mapigano makali ya siku kadhaa mwishoni mwa mwezi Julai.
Mjini Moscow, mita mia chache kutoka Kremlin, darzeni ya raia wa Russia walifika kuomboleza vifo vya wapiganaji wa Wagner, mwandishi wa shirika la habari la Reuters amesema.
Hakuna hata mmoja aliyeombwa kutoa maoni katika kumbukumbu alitaka kuzungumza na Reuters.
Mali, ambako mamlaka ya jeshi likamta madaraka katika mapinduzi ya mwaka 2020 na 2021, imekuwa katika mapigano ya muda mrefu na uasi wa kiislamu. Imesema vikosi vya Russia vilivyopo si mamluki wa Wagner lakini ni wakufunzi wanaowasaidia wanajeshi wa ndani kuhusu vifaa vilivyonunuliwa kutoka Russia.