Idadi ya vifo vya watoto vinaongezeka kutokana na vita Sudan

Watoto waliopoteza makazi kutokana na vita huko Sudan wakicheza nje ya shule ya sekondari ya Hasahisa ambako wanaishi. Picha na AFP

Idadi ya vifo vya watoto wenye mtapia mlo unaohushishwa na ukosefu wa makazi kutokana na vita katika jimbo la Darfur lililopo magharibi mwa Sudan imeongezeka sana, kulingana na matokeo ya utafiti wa shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF)

Tangu vita kuanza kati ya jeshi la Sudan na Kikosi cha wanamgambo cha RSF mwezi Aprili 2023, watu wapatao 300,000 wamekuwa wakiishi katika kambi ya Zamzam jirani na mji mkuu wa mkoa wa Darfur ya Kaskazini ambao haujakuwa ukipokea misaada ya kibinaadamu wala kuwa na uwezo wa kutoa huduma za afya.

Katika taarifa ya Jumatatu, MSF imesema inakadiria kuwa kuna vifo vya watoto takriban 13 kila siku, kulingana na tathimini ya dharura kuhusiana na lishe na vifo iliyofanywa Januari.

Waatalamu wanasema utapia mlo wao unatibika endapo, wataweza kufika katika vituo vya afya, lakini kutokana na upungufu wa msaada wa dharura, hali inazidi kuwa mbaya na kusababisha ongezeko la vifo.

Katika utafiti wa familia 400, MSF imegundua kiwango cha vifo 2.5 kwa kila watu 10,000 kwa siku katika kambi, mara mbili ya kiwango kilichozaniwa kuhitaji msaada wa haraka.

Ikiwa ni mtoa huduma pekee katika kambi ya Zamam, MSF imesema inalenga kuongeza haraka huduma zake kwa watoto ambao wako katika hali mbaya, lakini wamekubali kuwa tatizo hilo linahitiji rasilimali zaidi kuliko ujwezo wa shirika hilo hivi sasa, ikiwa ni pamoja na chakula, fedha, huduma za hospitali, maji na vifaa vya usafi.