Mafuriko ya hivi karibuni nchini Libya kufikia sasa yameua takriban watu 6,000 huku wengine wapatao 10,000 wakiwa wametoweka baada ya kusombwa hadi kwenye bahari ya Mediterranean au kufunikwa kwenye tope, serikali imesema Jumatano. Wakati huo huo, shirika la Kimataifa la Uhamiaji limesema kwamba mafuriko hayo mashariki mwa Libya yamekosesha makazi zaidi ya watu 30,000. Shirika hilo la kimataifa limesema kwamba wengi waliokoseshwa makao walikuwa wakiishi kwenye mji ulioharibiwa wa Derna, wakati maelfu wengine wakiwa ni kutoka maeneo mengine, ukiwemo mji wa Benghazi. Mabwawa mawili yalivunja kingo juu ya mji wa Derna na kuongeza mafuriko yaliokuwa yamesababishwa na mvua kutokana na kimbunga Daniel. Idadi kamili ya vifo huenda isijulikane kutokana na ushindani wa serikali mbili, baadhi ya maafisa wakisema kwamba huenda ikawa mara mbili.
Mafuriko ya hivi karibuni nchini Libya kufikia sasa yameua takriban watu 6,000 huku wengine wapatao 10,000 wakiwa wametoweka baada ya kusombwa hadi kwenye bahari ya Mediterranean au kufunikwa kwenye tope, serikali imesema Jumatano.