Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:22

Zimbabwe yajivunia mavuno ya tumbaku 2023, itaongeza kiwango cha mauzo yake nje ya nchi


Msimu wa mauzo ya tumbaku waanza Zimbabwe.
Msimu wa mauzo ya tumbaku waanza Zimbabwe.

Zimbabwe imezalisha kiwango kikubwa cha tumbaku  mwaka 2023 ikiwa ni tani 263,000 zimeuzwa katika kipindi hiki.

Wizara ya Kilimo imesema asilimia 85 ya uzalishaji unapatikana kutoka kwa wakulima wadogo ambao wengi wao walikuwa katika ardhi iliyo na mgogoro iliyochukuliwa zaidi ya miongo miwili iliyopita kutoka kwa wakulima wazungu chini ya sera ya kutatua tatizo la kuporwa ardhi kulikofanywa na ukoloni.

Kwa serikali hii ni uthibitisho wa uporaji wa ardhi wenye utata. Zimbabwe ni taifa kubwa la Afrika linalozalisha tumbaku na kusafirisha China, Mashariki ya Kati na Ulaya.

Mvua nzuri na msaada wa kifedha umesaidia wakulima kuweka rekodi hiyo ya uzalishaji.

Kwa mujibu wa mamlaka ya soko la tumbaku, usafirishaji nje wa zao hilo unatarajiwa kuongezeka zaidi wakati wakulima wanaendelea kupeleka katika masoko.

Tumbaku ni zao kuu la chanzo cha fedha za kigeni na limechangia kwa kiasi cha dola 800 kwa mwaka huu. Lakini linakuja kwa gharama kubwa kwa sababu ya mazingira ambapo wakulima wengi wanatumia kuni kutengeneza tumbaku ambapo inaweza kusababisha ukataji miti.

Watu wanapovuta tumbaku inaweza kusababisha hali mbaya ya kiafya ikiwemo aina mbalimbali ya saratani.

Forum

XS
SM
MD
LG