Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 20:35

Wizara ya mambo ya nje Zimbabwe yamhoji naibu balozi wa Marekani

Rais Emmerson Mnangagwa, wa Zimbabwe, alipohudhuria mkutano wa Hali ya Hewa wa Umoja wa Mataifa wa COP27, Novemba 7, 2022. (AP)
Rais Emmerson Mnangagwa, wa Zimbabwe, alipohudhuria mkutano wa Hali ya Hewa wa Umoja wa Mataifa wa COP27, Novemba 7, 2022. (AP)

Wizara ya mambo ya nje ya Zimbabwe imemwita naibu balozi wa Marekani kutokana na msururu wa ujumbe wa Twitter ambao ubalozi huo ulituma ukitaka uchaguzi ufanyike kwa amani katika nchi hiyo ambayo ina historia ya upigaji kura uliogubikwa na  vurugu na migogoro.

Wizara hiyo iliushutumu ubalozi huo kwa machapisho kwenye mitandao ya kijamii yanayohusiana na uchaguzi yanayoelekea kwenye uanaharakati na kuingilia masuala ya ndani ya Zimbabwe.

Naibu Balozi Elaine French aliitwa kwenye mkutano na kaimu katibu mkuu wa wizara ya mambo ya nje ya Zimbabwe Rofina Chikava Jumanne kufuatia machapisho kwenye akaunti rasmi ya Twitter ya Ubalozi wa Marekani.

Wizara ya mambo ya nje ya Zimbabwe ilisema ilitiwa wasi wasi na tweet ya Mei 26 iliyowataka Wazimbabwe Kujiandikisha kupiga kura na kuhakikisha sauti yao inasikika. Tweet nyingine kutoka kwenye ubalozi huo ilisema Katiba ya Zimbabwe inawapa raia haki ya kuchagua wawakilishi wao katika uchaguzi halali, unaoaminika na wa amani.

Forum

XS
SM
MD
LG