Mswaada huo ambao uliidhinishwa na bunge Jumatano jioni, unaharamisha vitendo vinavyohujumu “uhuru na maslahi ya taifa” ya nchi hiyo ya kusini mwa Afrika.
Wanaokiuka sheria hiyo wanakabiliwa hadi kifungo cha miaka 20 jela.
“Uhuru wa kujieleza umekufa,” mwandishi wa habari mashuhuri na mwanaharakati Hopewell Chin’ono ameandika kwenye Twitter, akiongeza kuwa ilikuwa “siku mbaya sana kwa Zimbabwe.”
Sheria hiyo ilipitishwa saa chache baada ya serikali kuondoa hali ya sintofahamu kwa miezi kadhaa, na kutangaza kwamba uchaguzi wa kitaifa utafanyika tarehe 23 Agosti.
Joseph Chinotimba, mbunge kutoka chama tawala cha ZANU-PF aliliambia bunge kwamba sheria hiyo mpya inalenga kuhamasisha Wazimbabwe kuwa “wazalendo.”
Lakini wapinzani wamesema inapiga marufuku ukosoaji wa serikali wakati ambapo makundi ya haki za binadamu na vyama vya upinzani tayari wamelalamika juu ya ukandamazaji.
Forum