Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 18:39

Mamlaka nchini Zimbabwe imewafungulia mashtaka wanaharakati 39 wa upinzani


Mfano wa wanaharakati wa upinzani Zimbabwe wakisimamiwa na polisi nchini humo. July 2020. (Columbus Mavhunga/VOA)
Mfano wa wanaharakati wa upinzani Zimbabwe wakisimamiwa na polisi nchini humo. July 2020. (Columbus Mavhunga/VOA)

Waendesha mashtaka wamesema kundi hilo lilishambulia ofisi ya chama tawala cha ZANU-PF, katika eneo la Nyatsime, kusini mwa mji mkuu, wiki iliyopita. Chama tawala cha ZANU-PF kimekuwa madarakani tangu uhuru mwaka 1980

Mamlaka nchini Zimbabwe zimewafungulia mashtaka wanaharakati 39 wa upinzani wanaoshutumiwa kuzua ghasia za kisiasa kuhusiana na madai ya kuharibu ofisi ya chama tawala siku ya Jumatatu wakati mvutano ukiongezeka kabla ya uchaguzi mkuu mwezi Agosti.

Waendesha mashtaka wamesema kundi hilo lilishambulia ofisi ya chama tawala cha ZANU-PF, katika eneo la Nyatsime, kusini mwa mji mkuu, wiki iliyopita. Chama tawala cha ZANU-PF kimekuwa madarakani tangu uhuru mwaka 1980.

Kundi hilo liliharibu nyumba kadhaa na pia kuwashambulia watu wa jamii ya Nyatsime na kusababisha uharibifu mkubwa wa mali na kusababisha majeraha makubwa kwao, waendesha mashtaka walisema.

Tukio hilo limekuja wakati makundi ya kutetea haki za binadamu na vyama vya upinzani nchini humo vikilalamikia kukandamizwa kuelekea uchaguzi mkuu. Mawakili wa watu waliokamatwa, hata hivyo, waliashiria kuwa mashtaka hayo yalichochewa kisiasa.

Forum

XS
SM
MD
LG