Zelenskyy ameisihi Marekani iendelee kuwataka washirika wake wa juu wa kimataifa kuendelea kumpatia msaada wa kijeshi na kiuchumi katika mapambano ya Ukraine dhidi ya uvamizi wa Russia.
Rais Joe Biden alimkaribisha Rais Volodymyr Zelenskyy huko White House jana Jumatano, katika ziara ya kushangaza ambayo ilipangwa kupeleka ujumbe kwa Rais wa Russia Vladimir Putin kwamba Marekani itakuwa pamoja na Ukraine kwa muda mrefu ujao.
Rais wa Marekani Joe Biden: “Yeye Rais wa Russia Vladimir Putin anajaribu kutumia majira ya baridi kama silaha, lakini watu wa Ukraine wanaendelea kuihamasisha dunia. Nasema hivyo kwa dhati kabisa. Siyo to kutuhamasisha sisi lakini pia kuihamasisha dunia kwa ujasiri na jinsi walivyochagua ustahmilivy wao na suluhu kwa siku za usoni.”
Zelenskyy alimshukuru Biden na kumpa medali ya msalaba wa sifa ya kijeshi ambayo ni ya mwanajeshi wa Ukraine, kapteni ya betri za HIMARS ambazo zilitolewa na Marekani.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alisema: “Yeye ni shujaa mkubwa. Na amesema, nimpe rais hii medali. Nataka kukupa huu msalaba wa sifa ya kijeshi.”
Zelenskyy alipotua kwenye ardhi ya Marekani kwa ziara yake ya kwanza nje ya nchi tangu uvamizi wa Russia mwezi Februari, Marekani ilitangaza msaada wa ziada wa dola bilioni 1.85 ikiwa ni msaada wa ulinzi kwa Ukaine, ikiwa pamoja na mfumo wa ulinzi wa Patriot ambao utasaidia kulinda dhidi ya makombora ya Russia – hatua ambayo Moscow inaiita ni ya ‘kichokozi.’
Jumatano, Putin alisema Russia haina “chochote cha kulaumiwa” katika vita.
Rais wa Russia,Vladimir Putin alieleza haya: “Kinyume na hivyo, haya ni matokoe ya sera za nchi nyingine, nchi za tatu, ambazo siku zote zimepania katika hili, kuelekea kuisambaratisha dunia ya Russia.”
“katika matamshi yake kwenye kikao cha pamoja cha bunge, Zelenskyy aliwaomba wabunge wa Marekani msada zaidi wakati ambapo wanajadili kuhusu msaada mwingine wa dharura wa dola bilioni 45 kwa Ukraine, ambao utafikisha idadi ya msaada wa Marekani wakati wa vita kufikia zaidi ya dola bilioni 100
Rais Zelenskyy amesema: “Fedha zenu si hisani. Ni uwekezaji katika usalama wa ulimwengu na demokrasia ambayo tunakabiliana nayo kwa njia ya uwajibikaji.”
Uksuanyaji maoni wa karibuni wa Baraza la Chicago umebaini kuwa wakati asilimia 65 ya wamarekani wanaendelea kuunga mkono msaada wa Marekani kwa Ukraine, wamegawanyika kati ya kusaidia “ kwa muda usio wa kikomo” na kuitaka Washington kuishi Kyiv kushughulikia upatikanaji wa amani haraka iwezekanavyo.