Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 11:31

Biden aahidi Zelenskyy uungaji mkono wa Marekani na washirika wake, wakati wa kikao chao mjini Washington


Rais wa Marekani Joe Biden akiwa na mwenzake wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy kwenye ikulu ya Marekani Jumatano
Rais wa Marekani Joe Biden akiwa na mwenzake wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy kwenye ikulu ya Marekani Jumatano

Rais wa Marekani Joe Biden Jumatano amemkaribisha mwenzake wa Ukraine Volodomyr Zelenskyy kwenye ikulu ya Marekani ,  ikiwa ziara yake ya kwanza  nje ya Ukraine tangu kuanza kwa uvamizi wa Russia dhidi ya taifa lake Februari mwaka huu.

Biden alisema kwamba watu wa Ukraine wameendelea kuhamaisha ulimwengu kutokana na ustahimilivu, pamoja na ushujaa wa kulilinda taifa lao. Ameongeza kusema kwamba watu wa Marekani wamesimama kwa majivuno na watu wa Ukraine.

Amsesema pia kwamba wademokrat na warepublican wako pamoja na washirika wao wa Ulaya na Japan pamoja na maeneo mengine, kuhakikisha kwamba Ukraine inapata misaada ya kifedha, kiusalama na kibinadamu inayohitajika.

Imekuwa ni siku 300 tangu Rais wa Russia Vladimir Putin alipoanzisha mashambulizi ya kikatili dhidi ya Ukraine, hatua inayolenga kuiondolea Ukraine haki ya kuwepo kama taifa.

Zelenskyy kwa upande wake alimshukuru Biden kutokana na msaada wake kwa Ukraine na watu wake, na kuelezea shukran zake za dhati kutoka moyoni na kutoka kwa waukraine wote.“Shukran, kutoka kwa watu wetu wa kawaida kuja kwa watu wako wa kawaida, wamarekani,” alisema.

Zelenskyy pia alimpa Biden medali ya msalaba wa kijeshi ambayo ilikuwa ya mwanajeshi wa Ukraine, kapteni wa betri za HIMARS, ambazo zilitolewa na Marekani.

Ziara yake imekuja wakati wabunge wa Marekani wanajadili msaada zaidi ya dharura wa dola bilioni 45 kwa Ukraine, ambao utafikisha jumla ya msaada wa Marekani wakati wa vita kuwa zaidi ya dola bilioni 100.

XS
SM
MD
LG