Shirika la Afya Duniani limesema janga la corona limesababisha vifo vya takriban watu milioni 15 kote duniani.
Hiyo ni zaidi ya asilimia 13 ya vifo ambavyo vilitarajiwa kwa miaka zaidi ya miwili.
WHO inaamini kwamba nchi nyingi hazikuhesabu vizuri idadi ya watu waliokufa kutokana na Covid, ni watu milioni 5.4 tu ndio walioripotiwa.
Nchini India kulikuwa na watu milioni 4.7 waliofariki kwa Covid, ikwa ni mara kumi zaidi ya idadi rasmi na takriban theluthi tatu ya vifo vya COVID ulimwenguni kote.
Hata hivyo serikali ya India imehoji makadirio ya idadi hiyo, ikisema kuwa ina wasiwasi kuhusu utaratibu uliotumika lakini utafiti mwingine unaonyesha kuwa sawa kuhusu viwango vya vifo nchini humo.
Utaratibu uliotumiwa na WHO unaonyesha ni kiasi gani cha watu zaidi wamekufa kuliko kawaida walivyotarajiwa kufuatana na taarifa ya vifo katika sehemu hiyo hiyo kabla ya janga la Covid.
Hesabu za vifo hivi zinaonyesha kuwa havikuwa vya moja kwa moja kwa sababu ya COVID na badala yake vimesababishwa na matokeo ya Covid , kama vile watu kushindwa kufika katika hospitali kwa ajili ya huduma wanazohitaji na pia zinatokana na uhifadhi mbaya wa rekodi katika maeneo , na vipimo vichache wakati janga lilipozuka.