Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 25, 2024 Local time: 16:51

Waziri wa ulinzi wa Ujerumani afanya ziara ya kushtukiza huko Ukraine


Waziri wa Ulinzi wa Ukraine Rustem Umerov akiwa na Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Boris Pistorius huko Kyiv, Novemba 21, 2023. Picha na REUTERS/Gleb Garanich
Waziri wa Ulinzi wa Ukraine Rustem Umerov akiwa na Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Boris Pistorius huko Kyiv, Novemba 21, 2023. Picha na REUTERS/Gleb Garanich

Afisa kutoka mshirika mwingine muhimu wa Magharibi amefanya ziara ya kushtukiza nchini Ukraine siku ya Jumanne wakati vikosi vya Russiai vikiendelea kushambulia miundombinu ya kiraia kwa makombora na ndege zisizo na rubani.

Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Boris Pistorius aliwasili mjini Kyiv siku moja baada ya ziara ya waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin.

Wawaziri hao wawili walisema mataifa yao yataisaidia Ukraine katika kipindi ambacha kinatarajiwa kuwa kirefu cha, baridi, na majira ya baridi kali yasiyo ya uhakika.

Ujerumani ni nchi ya pili kwa kutoa misaada ya kijeshi kwa Kyiv, baada ya Marekani.

Ziara ya pili ya Pistorius nchini Ukraine imekuja wakati wa kumbukumbu ya mapinduzi ya kidemokrasia ya Novemba 2013 nchini humo.

Katika hotuba yake siku ya Jumanne, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alihusisha maandamano ya 2013, ambayo yaliendelea kwa miezi kadhaa, na vita vilinyoendelea na Russia hivi leo.

Wakati huo huo, mashambulizi makubwa ya ndege zisizo na rubani na makombora ya Russia yaliendelea, na kuharibu hospitali, jengo lililoko kwenye mgodi na miundombinu mingine ya kiraia.

Katika ziara yake Jumatatu, waziri wa ulinzi wa Marekani alisema Pentagon itakuwa ikituma nyongeza ya dola milioni 100 za silaha kwa Ukraine, ikiwa ni pamoja na mizinga na zana za ulinzi wa anga.

Alisema juhudi za Ukraine kuvishinda vikosi vya Russia "ni muhimu kwa ulimwengu wote" na kwamba msaada wa Marekani utaendelea "kwa muda mrefu."

Forum

XS
SM
MD
LG