Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 25, 2024 Local time: 16:35

Waziri wa Ulinzi wa Marekani afanya safari ya kushtukiza nchini Ukraine


Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenzky (kulia) kabla ya mkutano na Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin (kushoto) huko Kyiv Novemba 20, 2023. Picha na AFP.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenzky (kulia) kabla ya mkutano na Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin (kushoto) huko Kyiv Novemba 20, 2023. Picha na AFP.

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin amefanya safari ya kushitukiza kwenda Kyiv siku ya Jumatatu katika kuonyesha mshikamano wa Magharibi, kuwahakikishia viongozi wa Ukraine kuwa Marekani itaendelea kuiunga mkono katika mapambano ya nchi yao dhidi ya uvamizi wa Urusi.

Austin alilakiwa katika kituo cha treni mjini Kyiv na balozi wa Marekani nchini Ukraine, Bridget Brink, na mwambata wa kijeshi wa Marekani, Brigedia Jenerali Kipling Kahler, na aliyejiunga katika ziara hiyo ni Jenerali wa Marekani Christopher Cavoli, ambaye anahudumu kama Kamanda Mkuu wa Muungano wa NATO Ulaya, na mkuu wa Kamandi ya Marekani Ulaya.

Maafisa wakuu wa ulinzi wa Merekani walisema Austin alikuja Kyiv kujadili mapambano ya dharura ya msimu wa baridi na kupanga misaada wa kiusalama kwa siku zijazo.

Ni ziara ya kwanza ya Austin tangu mwezi Aprili 2022, imekuja wakati msimu wa baridi unaanza na ambapo maafisa wa Ukraine na Magharibi wana imani kuwa Rais wa Russia Vladimir Putin ataanza tena kulenga miundo mbinu muhimu kama alivyofanya msimu uliopita wa baridi, na kuwaacha Waukraine wengi bila nishati kwa siku kadhaa za mwaka huo zilizokuwa na baridi zaidi.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenzky (kushoto) akimkaribisha Waziri wa Ulinzi wa Marekani Kyiv Novemba 20, 2023. Picha na AFP.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenzky (kushoto) akimkaribisha Waziri wa Ulinzi wa Marekani Kyiv Novemba 20, 2023. Picha na AFP.

"Moja ya kitu muhimu zaidi cha kufanya katika msimu huu wa baridi itakuwa ulinzi wa anga," afisa mkuu wa pili wa ulinzi aliwaambia waandishi wa habari wanaosafiri na Austin, na kuzungumza kwa masharti ya kutotajwa jina.

Mashambulizi ya takriban ndege zisizokuwa na rubani 40 zilizotengenezwa na Iran zilizorushwa kutoka eneo la Russia zilishambulia ulinzi wa anga wa Ukraine mwishoni mwa wiki.

Ukraine ilisema kuwa vikosi vyake viliharibu ndege 29 kati ya 38, lakini zile zilizofanikiwa kupitia ulinzi wa Ukraine ziliipiga miundombinu na kusababisha kukatika kwa umeme katika miji na vijiji zaidi ya 400 vya maeneo mbalimbali ya nchi.

Ndege hizo zisizo na rubani zilishambulia kuanzia mikoa ya Odesa na Zaporizhzhia kusini, hadi eneo la Chernihiv kaskazini, karibu na mpaka na Belarus.

Pia wameilenga Kyiv katika shambulio la pili hadi sasa kwa mwezi huu, lakini ndege zote zisizo na rubani zilizokuwa zikielekea katika mji mkuu zilitunguliwa, maafisa wa Ukraine walisema.

Forum

XS
SM
MD
LG