Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 22:03

Waziri wa Ulinzi: Mkataba wa nyambizi wenye utata utaimarisha uhuru wa Australia


Waziri wa Ulinzi wa Austrralia Richard Marles akikutana na Waziri wa Ulinzi Lloyd Austin huko Wizara ya Ulinzi ya Marekani- Pentagon, Feb. 3, 2023, in Washington.
Waziri wa Ulinzi wa Austrralia Richard Marles akikutana na Waziri wa Ulinzi Lloyd Austin huko Wizara ya Ulinzi ya Marekani- Pentagon, Feb. 3, 2023, in Washington.

Waziri wa Ulinzi wa Australia Richard Marles aliliambia bunge Alhamisi kuwa mkataba wenye utata wa nyambizi ya kivita aina ya AUKUS, kati ya Marekani na Uingereza, inaimarisha uhuru wa Australia, na haiongezi utegemezi wake kwa Marekani kama ilivyodaiwa na wakosoaji.

Mkataba huo ulisainiwa na Australia, Marekani na Uingereza mwezi Septemba 2021 lakini umelaaniwa na China.

Waziri Marles alisema kuwa kupokea angalau nyambizi nane zinazoendeshwa na nishati ya nyuklia chini ya mkataba wa AUKUS “zitaimarisha vilivyo” uhuru wa Australia na siyo kuidhoofisha.

Marles alisema kuwa Australia inahitaji utaalamu wa Uingereza na Marekani ili kuimarisha uwezo wake wa kijeshi.

China iliishutumu Australia, Uingereza na Marekani kwa kuchochea mivutano ya kijeshi wakati mkataba wa AUKUS ulipotiwa saini mwaka 2021.

XS
SM
MD
LG