Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 13:21

Baraza la Wawakilishi la Marekani lapitisha mswada unaowaruhusu wasafiri wa kigeni kuingia bila cheti cha Covid


Bunge la Marekani
Bunge la Marekani

Baraza la Wawakilishi la Marekani Jumatano lilipiga kura ya kuondoa utaratibu ambao unawataka wasafiri wote wa kigeni wanaosafiri kwa ndege kuonyesha kwamba walipewa chanjo dhidi ya Covid 19, mojawapo ya masharti machache ya kusafiri wakati wa janga la covid yaliyokuwa bado yanatekelezwa.

Mswada huo ulipitishwa na wabunge 227 dhidi ya 201, huku Wademocrats saba wakijiunga na Warepublican kwa kuupitisha.

Mwezi Juni, utawala wa Biden uliondoa masharti yake yanayowataka watu wanaowasili Marekani kwa ndege kuonyesha cheti kinachodhihirisha kwamba hawana Covid, lakini haukuondoa masharti ya kituo cha Marekani cha kuzuia na kudhibiti magonjwa (CDC) ya kuwataka wasafiri wa kigeni kupata chanjo ya Covid kabla ya kuingia Marekani.

White House Jumanne ilisema kwamba inapinga mswada huo.

XS
SM
MD
LG