Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 20:26

Watu zaidi ya watu 100 hawajulikani walipo Nigeria


Wasichana waliotekwa wakisubiri kuungana na familia zao katika jimbo la Zamfara Machi 3 2021. Picha na Aminu ABUBAKAR / AFP.
Wasichana waliotekwa wakisubiri kuungana na familia zao katika jimbo la Zamfara Machi 3 2021. Picha na Aminu ABUBAKAR / AFP.

Zaidi ya watu 100 hawajulikani walipo baada ya wanajihadi kaskazini mashariki mwa Nigeria kuwateka watu wengi wakiwalenga wanawake na watoto kutoka kwenye kambi za wasiokuwa na makazi, maafisa wameliambia shirika la AFP.

Viongozi wa wanamgambo wanaopinga jihadi wamelilaumu kundi la Islamic State la Afrika magharibi (ISWAP) kwa shambulizi la wiki iliyopita katika jimbo la BORNO eneo ambalo lina uasi mkubwa wa wana- jihadi ambao wamesababisha vifo vya zaidi ya watu 40,000 na kuwakosesha makazi wengine milioni mbili tangu mwaka 2009.

Taarifa za kina kuhusu shambulizi katika eneo la vijijini la ngala bado hazifahamiki na maafisa wametoa taarifa zinazokinzana. Idadi ya watu walioripotiwa kuwa hawajulikani walipo hailingani na ile ya watu wanaoshikiliwa mateka.

Ofisi ya umoja wa mataifa inayoshughulika na masuala ya kibinadamu – OCHA imesema shambulizi lilifanyika alhamisi wiki iliyopita na inakadiriwa kuwa watu 200 kutoka kwenye kambi za waliokoseshwa makazi wametekwa.

Imesema washambuliaji waliokuwa na sialaha waliwateka wanawake wakiwa nje wanatafuta kuni.

Forum

XS
SM
MD
LG