Katika mkutano na waandish wa habari Alhamisi, maafisa wa idara hiyo walisema kwamba wamefahamisha familia za watu waliokuwa ndani ya chombo hicho, kuhusu na mkasa huo.
Vifusi vilivyopatikana wakati wa utafutaji wa chombo hicho "vinaashiria ajali mbaya," alisema Admirali John Mauger. "Rambirambi zetu za dhati zinaenda kwa marafiki na wapendwa wa watu hao,” Mauger alisema.
Kampuni ya OceanGate Expeditions, inayomiliki chombo hicho, ilisema katika taarifa kwamba watu wote watano waliokuwa ndani, wakiwa ni pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Stockton Rush, wanaaminika kuwa wamekufa.
Vipande vitano tofauti viligunduliwa ambavyo viliruhusu mamlaka kuthibitisha kuwa vilitoka kwa Titan, ikiwa ni pamoja na sehemu ya nyuma ya chombo hicho. Kutoweka kwa chombo hicho kulipelekea juhudi kubwa za utafutaji wa kimataifa iliyohusisha vikosi vya Marekani, Kanada, Uingereza na Ufaransa.
Shughuli za kutafuta mili ya waathiriwa, zinaendelea.
OceanGate imekuwa ikirekodi hali ya kuoza kwa Titanic na mfumo ikolojia wa chini ya maji unaoizunguka kupitia safari za kila mwaka tangu 2021.
Forum