Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 06:32

Malaysia yaidhinisha uchunguzi mpya wa ndege iliyopotea 2014


Waziri wa Usafiri wa Malaysia Liow Tiong Lai (kati) akiongea katika mkutano wa waandishi wa habari juu ya uchunguzi wa ndege iliyopotea MH370
Waziri wa Usafiri wa Malaysia Liow Tiong Lai (kati) akiongea katika mkutano wa waandishi wa habari juu ya uchunguzi wa ndege iliyopotea MH370

Serikali ya Malaysia imesaini makubaliano na kampuni ya utafiti ya Marekani kuanza upya uchunguzi juu ya kupotea kwa ndege ya shirika la ndege la Malaysia MH370 katika upande wa kusini wa Bahari ya Hindi.

Waziri wa Usafiri Liow Tiong Lai ametangaza Jumatano huko Kuala Lumpur kuwa kampuni hiyo ya Ocean Infinity iliyoko Houston itaendele kuitafuta ndege hiyo iliyotoweka kwa mkataba wa “kama haijapatikana, hakuna malipo” ikimaanisha kuwa kampuni hiyo italipwa tu iwapo itaipata ndege hiyo Boeing 777.

Kampuni hiyo italipwa dola milioni 20 iwapo itapatikana na eneo la kilomita za mraba 5,000, dola milioni 30 iwapo itapatikana katika kilomita za mraba 10,000, na dola milioni 50 iwapo itapatikana katika kilomita za mraba 25,000 katika eneo lililotokea ajali hiyo. Malipo yatakuwa ni dola milioni 70 iwapo mabaki ya ndege hiyo iliyotoweka itapatikana nje ya kilomita za mraba 25,000.

Ndege ya Shirika la Malaysia MH370 ilitoweka Machi 8, 2014 wakati ikisafiri kutoka Kuala Lumpur kwenda Beijing, ikiwa na abiria 239 na wafanyakazi wake.

XS
SM
MD
LG