Pendekezo hilo lilitolewa siku ya Jumanne wakati wa mkutano wa kwanza wa ana kwa ana katika kipindi cha miaka miwili kati ya nchi hizo mbili hasimu.
Naibu waziri wa ushirikaiano, Chun Hae Sung aliwaambia waandishi wa habari mjini Seoul kwamba Korea Kaskazini itatuma maafisa wa ngazi za juu, wanariadha na kikundi cha washangiliaji kwenye micheo hiyo itakayoanza Februari 9.
Aidha waziri huyo alisema Korea Kusini imependekaza mkutano mwingine wa kuziunganisha familia zilizotenganishwa na vita vya kati ya mwaka wa 1950 na 1953, ambavyo vilitenganisha nchi hizo mbili, ufanyike mwezi ujao.