Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 04:59

Watu 61 wafariki katika ajali ya boti


Wahamiaji wakiwa wameketi kwenye boti ya ulinzi wa bahari ya Italia wakisubiri kushuka katika bandari ya Palermo, baada ya kuokolewa Jumamosi, Aprili 18, 2015. Picha na shirila la habari la AP/Alessandro Fucarini.
Wahamiaji wakiwa wameketi kwenye boti ya ulinzi wa bahari ya Italia wakisubiri kushuka katika bandari ya Palermo, baada ya kuokolewa Jumamosi, Aprili 18, 2015. Picha na shirila la habari la AP/Alessandro Fucarini.

Idadi ya wahamiaji waliokufa baada ya boti yao kupata ajali kusini mwa pwani ya Italy, imefikia watu 61.

Maafisa wanaendelea kuwatafuta watu wengine waliozama baada ya ajali hiyo.

Boti iliyotengenezwa kwa mbao, ilikuwa imebeba wahamiaji kuelekea Ulaya kutokea Uturuki.

Iliharibika mapema Jumapili baada ya kugonga miamba karibu na Steccato di Cutro, mashariki mwa pwani ya Calabria.

Watu 61 wamethibitishwa kufariki na 80 wameokolewa.

Boti hiyo ilikuwa imebeba watu kutoka Afghanistan, Iran na nchi nyingine. Miongoni mwa waliofariki ni watoto 12.

Kulingana na watu walionusurika, boti hiyo ilikuwa imebeba kati ya watu 180 na 200.

Mtu mmoja, aliyenusurika kifo amekamatwa kwa kufanya biashara ya kusafirisha watu na maafisa wa polisi wa forodha wamesema kwamba wanakamilisha mchakato wa kuwakamata watu wengine wawili kwa kushiriki katika kusafirisha watu kinyume cha sheria.

XS
SM
MD
LG