Ziara ya Macron inajiri baada ya Ufaransa kukumbana na changamoto za kijeshi na kisiasa katika nchi washirika barani Afrika, katika siku za karibuni.
Macron atatembelea nchi za Congo Brazaville, Gabon, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na Angola.
Ziara yake inajiri wakati kuna matamshi ya chuki dhidi ya Ufaransa katika eneo la Sahel.
Burkina Faso iliwafukuza wanajeshi wa Ufaransa wiki chache zilizopita na kumaliza ushirikiano wake wa kijeshi na Ufaransa katika kupambana na makundi ya wanajihadi katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.
Burkina Faso inakuwa nchi ya hivi punde kukataa msaada wa Ufaransa, ambayo iliwaondoa wanajeshi wake kutoka Mali mwaka uliopita baada ya viongozi wa kijeshi kuanza ushirikiano na mamluki kutoka Russia na kumaliza muongo mzima wa operesheni zake dhidi ya waasi wa kiislamu.