Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 18:15

Watu 15 wauawa katika shambulizi Burkina Faso


PICHA YA MAKTABA: Maafisa wakilinda doria katika eneo linaloshuhudia mashambulizi ya mara kwa mara.
PICHA YA MAKTABA: Maafisa wakilinda doria katika eneo linaloshuhudia mashambulizi ya mara kwa mara.

Takriban raia 15 waliuawa Jumatano na watu wanaoshukiwa kuwa wanajihadi nchini Burkina Faso, na kusababisha mmiminiko wa watu kuondoka kwa makazi yao wanaohofia umwagikaji damu zaidi, vyombo vya usalama na vya ndani vililiambia shirika la habari la AFP.

Shambulio hilo lilithibitishwa na mkazi mmoja wa eneo hilo pamoja na vyanzo vya usalama.

Burkina Faso, mojawapo ya mataifa maskini zaidi duniani, inapambana na uasi wa wapiganaji wa kiislamu ambao ulianzia nchini Mali mnamo mwaka wa 2015, na imeshuhudia zaidi ya raia 10,000, wanajeshi na polisi wakiuawa, kulingana na takwimu za shirika moja lisilo la serikali,

Takriban watu milioni 2 wamelazimika kuyahama makazi yao.

Hasira ndani ya jeshi kwa kushindwa kudhibiti uasi huo, zilisababisha mapinduzi mawili nchini Burkina Faso mwaka jana.

Mashambulizi manne ya watu wanaoshukiwa kuwa wanajihadi nchini Burkina Faso yaliwauwa wanamgambo 40 wa kujitolea, na wanajeshi 39 wa kawaida wiki iliyopita, jeshi na vyanzo vya usalama vilisema.

Mapigano mawili mabaya zaidi yalitokea katika eneo la Centre-Nord mnamo tarehe 26 mwezi Juni na taarifa za awali zilielezea kwamba darzani za watu walikuwa wameuawa.

Forum

XS
SM
MD
LG